Jumatano , 14th Jul , 2021

Mkuu wa wilaya ya Rorya Juma Chikoka, ametoa siku 30 kwa Halmshauri ya wilaya hiyo kuhakikisha inajenga vyoo katika eneo la soko la wafanyabiashara wa samaki na dagaa katika Kijiji cha Kengwa kwani soko hilo halina vyoo kwa takribani miaka 10 sasa.

Mkuu wa wilaya ya Rorya Juma Chikoka

DC Chikoka ametoa kauli hiyo alipotembelea soko hilo na kukuta hakuna huduma ya choo kwa takribani miaka kumi na soko hilo lipo pembezoni mwa Ziwa Victoria.

Wafanyabiashara wa soko hilo wamedai kwamba kukosekana kwa choo hicho kunaweza   kusababisha mlipuko wa magonjwa kwa kuwa wako karibu na Ziwa.

Kwa upande wake  Mwenyekiti wa Kijiji cha Mkengwa Mauna Iddy, amesema kuwa wataalaamu wa Halmshauri walishafika kijijini hapo na kukutana na serikali ya Kijiji kwa ajili ya kutatua changamoto hiyo lakini mpaka sasa hakuna huduma ya choo licha ya kukusanya mapato zaidi ya shilingi milioni 10 kila mwezi kutoka katika soko hilo.