Alhamisi , 23rd Mei , 2019

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeazimia kumsamehe Mbunge wa Shinyanga Mjini, Stephen Masele kufuatia kukutwa na hatia ya kulidharau Bunge huku Kamati ya Maadili ikipendekeza kufungiwa mikutano mitatu.

Uamuzi wa kumsamehe Mbunge Masele umependekezwa na Spika Ndugai baada ya kusomwa kwa hukumu ya Kamati ya Maadili iliyowasilishwa mapema leo asubuhi na Mbunge Almasi Maige.

Akizungumzia hukumu hiyo, Spika Ndugai alipendekeza bungeni Spika Wa Bunge kumsamehe Mbunge Masele, na kueleza kuwa amepokea taarifa ya Mbunge huyo kutaka kuomba radhi.

"Nitumie nafasi hii kuomba radhi kwa Viongozi wangu wote waliopata usumbufu katika sakata hili akiwemo Rais Magufuli, sikuchonganisha mihimili, bali nilikata rufaa baada ya Spika kuniandikia barua ya kunisimamisha bila hata ya kuniuliza lolote", amesema Masele.

Masele alikuwa akituhumiwa kwa makosa ya kulidharau Bunge na kudharau Mamlaka ya kiti cha Spika.