
Kushoto ni Spika wa Bunge Job Ndugai na kulia Mbunge wa Ukonga Jerry Silaa.
Kibali hicho kimeombwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Emmanuel Mwakasaka, na kwamba kibali hicho kitakapotolewa itabidi Mbunge huyo akamatwe na kufikishwa mbele ya kamati kesho Agosti 27, 2021, majira ya saa 4:00 asubuhi.
Mbunge hiyo aliitwa mbele ya kamati hiyo kwa ajili ya kujibu tuhuma mbalimbali yakiwemo makosa ya kusema uongo na kushusha heshima na hadhi ya Bunge na atakapofikishwa mbele ya kamati na Polisi atakabiliwa na kosa la kuidharau kamati.