Jumatano , 29th Apr , 2015

Waziri wa Fedha na Uchumi Tanzania Mh. Saada Mkuya Salum amesema serikali imeanza kuchukua hatua za haraka kuhakikisha shilingi ya Tanzania haiendelei kuporomoka ikiwemo kuimarisha maeneo maalum ya kuzalisha bidhaa za kuuza nje.

Waziri wa Fedha na Uchumi nchini Tanzania Mh. Saada Mkuya Salum.

Waziri wa Fedha na Uchumi Tanzania Mh. Saada Mkuya Salum amesema serikali imeanza kuchukua hatua za haraka kuhakikisha shilingi ya Tanzania haiendelei kuporomoka ikiwemo kuimarisha maeneo maalum ya kuzalisha bidhaa za kuuza nje, na maeneo maalum ya uwekezaji kiuchumi.

Akiwasilisha mapendekezo ya mfumo wa mapato na matumizi ya serikali kwa mwaka 2015 / 2016 kwa wabunge wa bunge la Tanzania Jijini Dar es salaam leo, Mh. Saada Mkuya amewataka watanzania kuzitumia fursa hizo ili kuongeza mauzo ya nje ya nchi sambamba na kupunguza uagizaji wa bidhaa na huduma zisizo za lazima kutoka nje ili thamani ya shilingi iendelee kuimarika.

Katika hatua nyingine waziri wa fedha na uchumi Mh. Saada Mkuya amesema mfumo wa bajeti kwa mwaka 2015 / 2016 imezingatia sera za uchumi pamoja na misingi na sera za bajeti ambapo sura ya bajeti inaonesha kuwa jumla ya shilingi trilioni 22, bilion 480 milioni 375 .6 ambayo imetoa vipaumbele mbalimbali zinatarajiwa kukusanywa na kutumika katika kipindi hicho.

Mh. Mkuya amesema kwa upande wa matumizi katika mwaka serikali imepanga kutumia jumla ya shilingi bilioni 22,000 milioni 480,000 kwa matumizi ya kawaida na maendeleo na kati ya fedha hizo sh. bilioni 16,000 milion 711,200 zimetengwa ajili ya matumizi ya kawaida.