Jumatatu , 22nd Nov , 2021

Jeshi la Polisi mkoa wa Ruvuma limekanusha taarifa zilizosambaa mitandaoni zikieleza kwamba kanisa katoliki la parokia ya Mpitimbi lililopo wilaya ya Songea mkoani humo limechomwa moto baada ya Padri wa kanisa hilo kukataa kuendesha ibada ya mazishi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Joseph Konyo

Akielezea tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Joseph Konyo, amesema taarifa zilizosambazwa mitandoni ni za uongo, na kusema kwamba kilichofanyika ni vijana wenye nia ovu kwenda kupanga magogo katika milango ya kanisa hali iliyozua taharuki kwa wananchi

Aidha, Kamanda Konyo ameeleza kwamba Padri alikataa kuendesha ibada ya mazishi ya marehemu huyo kwa madai ya kwamba marehemu alikuwa akiishi unyumba na mume wa mtu.