
Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA katika Wizara ya Nishati na Madini, Francis Fungameza amesema kuwa ili mteja aweze kupata huduma hiyo anatakiwa kuandika neno MEM, ache nafasi , kisha aandike Namba ya Leseni na kutuma kwenda 15341.
Fungameza alisema kuwa hizo ni habari njema kwa wamiliki wa leseni kwani sasa wataweza kupata taarifa hizo kwa wakati na hivyo kulipia ada za leseni hizo kwa wakati.
Aidha Fungameza alisema kuwa Wizara imekuwa ikibuni njia mbalimbali ili kuhakikisha kuwa huduma za utoaji wa leseni za madini pamoja na taarifa mbalimbali kuhusu leseni hizo zinapatikana kwa urahisi na uharaka tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Fungameza alieleza kuwa hapo awali, mfumo wa utoaji leseni ulifanyika kwa njia ya mkono (manually) na ulitegemea utumaji wa karatasi (paperwork based) na hali hiyo ilichangia kuchelewesha utoaji leseni na kuongeza kuwa utoaji huo wa leseni ulitegemea hali ya mawasiliano kama ya telegram na rejesta.