Jumanne , 24th Jan , 2023

Mamlaka ya Korea Kaskazini imeonya juu ya hali mbaya ya hewa nchini humo wakati wimbi baridi kali likiikumba rasi ya Korea.

Viwango vya joto huenda vikapungua chini ya nyuzi joto -30 katika mikoa ya kaskazini, ambayo pia ni sehemu maskini zaidi ya nchi, kituo cha redio cha serikali kimesema.

Maeneo ya Pwani pia yanatarajiwa kushuhudia upepo mkali, kulingana na vyombo vya habari vya serikali.Korea Kusini pia imetoa tahadhari ya wimbi baridi na kaskazini mwa China imekuwa ikikabiliwa na rekodi ya joto la chini.

Viwango vya joto pia vinatarajiwa kushuka hadi chini kabisa katika kipindi cha muongo mmoja nchini Japani wiki hii.

 Ryanggang, North Hamgyong na South Hamgyong, majimbo maskini zaidi nchini humo na yale yanayotarajiwa kuwa hatarini zaidi kwa mshtuko wa hali ya hewa, yote yapo kaskazini mwa nchi hiyo.