Jumanne , 10th Mei , 2016

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini Tanzania (Takukuru) imebaini shehena ya tani 1,840 za sukari ambazo zilikuwa zimehifadhiwa kwenye makontena 70 yaliokuwa bandarini kwa takribani zaidi ya miezi mitatu.

Akiongea katika zoezi la kufungua makontena hayo Kaimu Mkurugenzi wa Uchunguzi (TAKUKURU) Leonard Mtalai amesema kuwa walipofanya uchunguzi wamebaini kuwa sukari hiyo inamilikiwa na AL Naem Zacharia ambae alinunua mzigo huo bandarini baada ya kushindikana kusafirishwa kwenda Burundi.

Kawa upande wake Meneja wa Kampuni iliyoaagiza mzigo huo Haroon Daudi Zacharia amesema kuwa kwa kipindi chote hicho walikuwa wanashindwa kuingiza sokoni sukari hiyo kwa kile walichokidai kuwa ni kufuatilia vibali na kodi za TRA.

Nchi ya Tanzania inakabiliwa na upungufu mkubwa wa sukari kwa takribani mwezi sasa huku bei ya sukari chache iliokuwa inapatikana ikiuzwa kwa bei kubwa tofauti na bei iliyoelekezwa na serikali.