Jumamosi , 8th Aug , 2020

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), imekamilisha uchunguzi wake na kugundua kuwapo ubadhirifu na migongano ya kimaslahi baada ya tume iliyoundwa na Brigedia Jenerali John Mbungo kuchunguza ujenzi wa majengo Saba ya ofisi za taasisi hiyo katika wilaya Saba kukamilika

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo

Hayo yamesemwa Brigedia Jenerali Mbungo  katika ofisi mpya za Takukuru zilizopo Mpwapwa ambapo amesema kuwa wahusika wote watachukuliwa hatua ikiwamo kufikishwa mahakamani.

Hayo yanajiri baada ya Rais John Magufuli kugundua kuwa si kweli kuwa shilingi milioni 143 zimetumika kujenga ofi si ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa wakati akifungua ofisi za Chamwino Julai 23. 

Baada ya siku kadhaa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo aliwasimamisha watumishi wa taasisi hiyo  ili kupisha uchunguzi na aliwataja waliosimamishwa kuwa ni Jarudi Nyakongeza na Adam Mandia.

Wengine ni Fortunatus Ngailo, Mohamed Kichewele, Nathaniel Otieno, Wilhelm Chuwa, Hamisi Masoud, Mbwana Malumbo na Benedict Mabula.