Jumatano , 30th Sep , 2020

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), imewaonya wale wote wanaojihusisha na vitendo vya kuwarubuni wapiga kura kadi zao kuacha tabia hiyo mara moja kwani hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Hayo yamesemwa leo na Afisa Habari wa TAKUKURU Doreen Kapwani, ambapo amesema TAKUKURU itachukua hatua kali ikiwemo kuwafikisha mahakamani wahusika.

Inadaiwa kuwa wananchi wanaorubuniwa ni wale waliojiandikisha kwenye daftari la mpiga kura ambao huahidiwa kupewa fedha, mikopo  na kutunziwa kadi zao hizo hadi 28 Oktoba.

Aidha TAKUKURU inakemea vikali vitendo hivyo ambavyo ni kinyume cha sheria zinazosimamia uchaguzi na ikwemo Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 1985 na ya kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.