Jumatatu , 29th Jun , 2020

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imesaini mikataba mitatu yenye thamani ya Zaidi ya TSh. Bilioni 590 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya maji, umeme vijijini Kusini mwa Tanzania.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Doto James emesema lengo la Serikali kusaini mikataba hiyo ni kuongeza uboreshaji wa miradi mikubwa iliyodhamiria kuchagiza shughuli za maendeleo kwa Watanzania.

Amesisitiza kuwa ili kukuza uchumi kwa Watanzania wanaoishi vijijini, ni muhimu kuweka mkazo kwenye miradi ya maji na umeme kwakuwa ni huduma muhimu.

Kwa upande wake Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier amesema anaipongeza sana Tanzania kwa uwekezaji mkubwa ilioufanya kwenye sekta ya maendeleo hasa katika miundombinu ya Barabara.

Mikataba hii iliyosainiwa leo inaendelea kutekeleza Dira ya maendeleo ya mwaka 2020-2025 ukiwa ni mpango wa awamu ya pili.