Jumanne , 3rd Mei , 2016

Wizara ya jenzi,Uchukuzi na Mawasiliano kupitia wakala wake wa ufundi umeme nchini Tanzania TEMESA umesimamisha huduma za kivuko cha mv Magogoni kwa muda ili kiweze kufanyiwa matengenezo makubwa kutokana na kivuko hiko kuwa na viashiria vya uchakavu

Akiongea na waandiashi wa habari ofisini kwake Kaimu Mtendaji Mkuu wa TEMESA Mhandisi Manase Olekujam amesema kuwa kivuko hiko kimeonekana kuwa na kutu katika baadhi ya maeneo na kutoboka baadhi ya vyuma hivyo wameamua kukifanyia ukarabati wa kina kisije leta madhara hapo baadae.

Aidha amesema kwa sasa wakati kivuko hicho kinafanyiwa matengenezo serikali imekodisha kivuko kingine kitakachokuwa kinabeba abiria pekee ili kiweze kusaidiana na kivuko kilichopo cha mv Kigamboni lakini kwa wanaotumia magari binafsi wameshauriwa kutumia daraja la Mwl Nyerere mpaka pale kivuko kitakapotengemaa.