Ijumaa , 13th Mar , 2015

Kituo cha uwekezaji nchini Tanzania TIC kimesema migogoro inayoendelea nchini kati ya wawekezaji na wananchi ni matokeo ya ukiukwaji wa makubaliano ambayo wawekezaji wanatakiwa kutimiza kwa wananchi.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa na mwenzake waziri mkuu wa Jamhuri ya watu wa China.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam na afisa ardhi wa TIC, Bw. Ildefonce Ndamela wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu mambo mbalimbali katika uwekezaji wa kilimo kwa wawekezaji hapa nchini.

Aidha katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa idara ya mahusiano ya Asia na Australia kutoka wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa nchini Tanzania, Balozi Mbelwa Kairuki amesema kuwa Tanzania ina nafasi kubwa katika ushirikiano wa kibiashara baina yake na China Mbali na kuwepo kwa uvumi unaovumishwa na Nchi jirani ya Kenya kuhusu Tanzania kususwa na nchi ya China kibiashara.

Balozi Kairuki ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akiongelea uwekezaji mkubwa unaotarajiwa kufanywa na wawekezaji kutoka nchini China na Tanzania kufanywa kuwa kitovu cha uwekezaji huo mkubwa katika ukanda wa Afrika.