Jumamosi , 18th Apr , 2015

Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es salaam imeyataka mashirika yasiyo ya kiserikali kutoa elimu kwa wananchi juu ya ugonjwa wa kifua kikuu na kuwaeleza kwamba ugonjwa huo unatibika na wasione aibu kwenda hospitali pale wanapoona dalili zake.

Naibu Meya Manispaa ya Kinondon,Songoro Mnyonge (katikati), akiongea.

Ushauri huo umetolewa na Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge wakati wa wadau wa afya kwa lengo la kujadili changamoto za sekta ya afya kwa upande wa ugonjwa wa kifua kikuu.

Naibu Meya Songoro Mnyonge amesema baadhi ya wananchi wamekuwa na aibu kwenda hospitali licha ya kuwa na dalili zote za kuugua kifua kikuu.

Mnyonge amesema kupitia asasi zisizo za kiserikali na mashirika mbalimbali zina wajibu sasa wa kuelimisha jamii kwamba ugonjwa wa kifua kikuu unatibika.