Jumamosi , 19th Nov , 2016

Mwanasheria Mkuu wa jimbo la New York nchini Marekani amesema rais mteule wa Marekani Donald Trump amelipa fidia ya dola milioni 25 kufuatia mashauri matatu yaliyofunguliwa dhidi yake kufuatia utapeli wa chuo kikuu cha Trump

Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump

Trump alishitakiwa na wanafunzi wa zamani waliosoma katika chuo hicho ambao walidai kutapeliwa na chuo hicho.Mwanasheria Mkuu wa New York  Eric Schneiderman amesema kulipwa kwa fidia hakukutarajiwa kufanywa na Trump na ni ushindi mkubwa kwa  wahanga wa chuo hicho.

Trump alifunguliwa mashitaka ya madai na wanafunzi hao kwa tuhuma za kuwapotosha na kushindwa kutimiza ahadi zilizotolewa na chuo hicho huko  California na  New York.