
Pichani: Mkuu wa Wakala wa Usalama na Miundombinu (Cisa),Christopher Krebs
Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa amemfuta kazi Mkuu wa Usalama wa Mtandao na Shirika la Usalama wa Miundombinu ya Uchaguzi (Cisa), Christopher Krebs, kwa kupinga madai yake juu ya ulaghai na wizi wa kura kwenye uchaguzi wa Novemba 3.
Kufukuzwa kwa Krebs kunakuja wakati Trump akiendelea kukataa kuyatambuwa matokeo ya uchaguzi huo ambao mpinzani wake mkuu kutoka chama cha Democrat, Joe Biden, alishinda huku akitoa madai yasiyothibitishwa ya udanganyifu mkubwa wa wapiga kura hata hivyo maafisa wa uchaguzi wanasema upigaji kura wa mwaka huu ulikuwa salama zaidi katika historia ya Amerika
Krebs si afisa wa kwanza anayeshuku madai ya Trump kufutwa kazi wiki iliyopita alimfukuza kazi, Waziri wa Ulinzi, Mark Esper ,katika juhudi za kuweka watu wanaomtii kwenye nafasi za juu ya wizara hiyo.
Krebs ndiye aliyekuwa akiliongoza shirika hilo la usalama wa mitandaoni tangu lilipoanzishwa mara tu baada ya uchaguzi wa 2016.