
Trump na Putin walizungumza kwa pamoja jukwaani kwa takriban dakika 10 baada tu ya kutoka kwenye mazungumzo yao yaliyokuwa yanasubiriwa na dunia nzima
Wote wawili walionesha ishara ya mazungumzo mema waliokuwa nayo wakati wa mkutano wao wa faragha, ingawa ulimalizika bila makubaliano madhubuti.
Putin ameuelezea mkutano huo kama mahali pa kuanzia kwa utatuzi wa mzozo na Ukraine huku akisema uhusiano wake na Trump ni imara na kukubaliana na madai ya mara kwa mara ya rais wa Marekani kwamba vita haingeanza ikiwa angesalia madarakani baada ya uchaguzi wa 2020.
Kwa upande wake, Trump alisema bado kuna mambo ambayo hawajakubaliana na hakuna makubaliano hadi maafikiano yawepo na kuongeza kuwa hawakufikia walipotaka ila wamepiga hatua kubwa. #EastAfricaTV