Jumamosi , 25th Mei , 2019

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Watanzania watumie Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kudumisha amani na mshikamano na kuwaombea viongozi wa kitaifa.

Waziri Mkuu alitoa wito huo jana jioni (Ijumaa, Mei 24, 2019), aliposhiriki hafla ya futari iliyoandaliwa na benki ya NMB iliyofanyika katika Hoteli ya Dodoma.

Alisema kila mwananchi aendelee kuliombea taifa lizidi kudumisha amani na mshikamano. “Tuhakikishe tunatenda matendo mema yenye kumpendeza Mwenyezi Mungu.”

Mwezi huu tuna majukumu makubwa ya kufanya ibada, kutubu dhambi zetu na kuomba rehma kwa Mwenyezi Mungu pamoja na kudumisha mshikamano na kuwa wavumilivu.” amesema Waziri Mkuu.

Kwa sasa waumini wa dini ya Kiislamu wapo kwenye ibada ya mfungo wa ramadhani ambapo wanafunga kwa siku 30.