
Waziri Simbachawene ametoa kauli hiyo katika mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao (Zoom) na kuwakutanisha wadau mbalimbali wa vyama vya siasa ambapo amesema kuwa katazo la mikutano ya kisiasa nchini halikuja kwa bahati mbaya bali ilikuwa ni kutona na hali ya kisiasa iliyokuwepo kwa wakati huo
"Marufuku ya mikutano ya hadhara haikuja tu, ilikuja baada ya kuona kuna matokeo hasi, tulimaliza uchaguzi, serikali iliyochaguliwa kihalali ikaingia kutekeleza yale iliyoahidi, sasa ilitokea vile kwa sababu kidogo vuguvugu la uchaguzi linapokuwa bado moto wake ni mkali, vyama vikataka kuingia barabarani, busara ya wakati huo tukaweka zuio kwa muda"
Amewashauri viongozi wa vyama wa siasa nchini kufanya siasa za kistaarabu zisizokuwa na matusi huku akieleza kuwa upinzani wa Tanzania miaka ya nyuma ulijengwa kwa hoja za ufisadi na kuzungumza masuala ya maadili ya viongozi na sio matusi
"Vyama vya ushindani vinavyoshindana na chama tawala vilipata kujengwa katika nchi hii wakati wa masuala ya ufisadi, ambayo yalikuwa yanaibuliwa ndani na nje ya bunge, haya mambo yakisemwa sio matusi, lakini yana nguvu kubwa na ndio ualiyijenga vyama vya upinzani"
Akichangia katika mjadala huo Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendio Zitto Kabwe amesema kuwa ni busara kumpongeza Rais wa Tanzania kwa kuondoa katazo hilo huku akisema kumpongeza kutampa nguvu ya kufanya mabadiliko mengine mbalimbali nchini
"Ni kweli kwamba aliyezuia mikutano anatokana na CCM na aliyeruhusu anatokana na CCM, lakini nadhani kupongeza ni uungwana kwamba kama mtu amerekebisha makosa ya mwenzie unampongeza na kumpa moyo ili afanye zaidi"
"Rais ameondoa lile zuio la mikutano ya hadhara, kwanini msimpongeze, ni kweli kwamba mikutano ya hadhara ni haki kikatiba
Aidha John Mrema kutoka Chama cha Demokrasia na Meendeleo chadema amesema kuwa Chama hicho kimepokea kwa furaha Tangazo hilo la Rais Samia na kueleza kuwa ni wakati wa kufanya siasa za kistaarabu huku mwanasiasa mkongwe nchini Sephen Wasira akisisitiza kuwa maendeleo ya nchi yoyote yanaanza na amani na utulivu wa nchi yenyewe
"Kuondolewa kwa hili zuio ni suala ambalo CHADEMA tumelipokea, na tutatumia fursa hiyo kwenda kuzungumza na wananchi ambao kwa miaka takribani saba sasa hatukupata fursa ya kukutana nao ana kwa ana lakini tulikuwa na fursa ya kutumia njia ya mitandao" amesema John Mrema ambaye ni Mkurugenzi wa mawasiliano, Itifaki na mambo ya nje wa CHADEMA
"Amani lazima iwe msingi wetu mkubwa, hakuna nchi ambayo inaweza ikapata maendeleo kama hakuna amani na unaweza ukafanya maendeleo hata kama hakuna demokrasia na inategemea vilevile unavyodefine demokrasia, ziko nchi ambazo zimefanya maendeleo bila kuwa na mfumo wa vyama vingi" - amesema Wasira