Jumanne , 15th Nov , 2022

Serikali wilayani Ilemela mkoani Mwanza imewaonya vijana wasio waaminifu ambao wamekuwa wakijiunga kwenye makundi ya uhalifu kama panya road na kusema atakayejaribu kufanya hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Kaimu Mkuu wa wilaya ya Ilemela Salum Kalli

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkuu wa wilaya ya Ilemela Salum Kalli, wakati akifunga mafunzo ya awali ya vijana wa jeshi la akiba na kuwataka kuyatumia mafunzo waliyopewa kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na siyo kuchochea vitendo vya uhalifu

"Nina imani kwamba katika mitaa yetu 171 mnaenda kuwa walinzi wazuri hatutakubali kuona namna nyinyi mmejifunza tukapata panya road huko na mimi niwatangazie kupitia Mstahiki Meya na Mwenyekiti wa chama sisi panya road Ilemela marufuku ndiyo maana nyinyi mpo hapa mmeiva vizuri, tunataka wananchi wa wilaya ya Ilemela waanike nguo nje na kuacha sufuria kesho aikute salama ndipo tutaona mafunzo yamekamilika vizuri" amesema Mh Kalli.

Jumla ya vijana 75 wamehitimu mafunzo hayo ya jeshi la akiba.