
Dr Nyimbi atoa rai mara baada ya kuzikabidhi mizinga ya nyuki iliyotolewa na Waziri wa maliasili na utalii Dr Pindi Chana kwa jumuiya za UWT za wilaya za mkoa wa Njombe ambapo amesema kumekuwa na tabia ya wanachama na makatibu ambao wametanguliza mbele maslahi binafsi na kisha kuwapa dhamana ya kugombea na kuongoza wanachama wapya bila kujua dhamira yao na kudai kwamba kitendo hicho kinavunja moyo kwa wanachama wenye nia ya kuongoza baada ya kupigania chama nyakati mbaya na nzuri
Akizungumzia kuhusu mradi wa Nyumba ya katibu wa UWT wilaya ya Njombe uliyogharimu zaidi ya mil 40 Katibu huyo wa UWT Taifa amesema itasaidia kwa mtumishi huyo kutekeleza majukumu yake bila kikwazo na kisha kushindwa kuzuia hisia zake kwa kitendo cha waziri wa maliasili na Utalii nchini kwa kuzipa jumuiya zote za UWT za mkoa huo Pikipiki na mizinga ya nyuki kwa lengo la kuziongezea kipato.
Mara baada ya kuzindua mradi wa nyumba wenye thamani ya mil 41 ndipo wana UWT akiwemo waziri wa maliasili na utalii Balozi Dr Pindi Chana wanakatoa hisia zao kwanini wamekuwa wakibuni miradi ya uchumi kila uchwao zikwemo Nyumba na vibanda vya biashara.