Jumanne , 18th Nov , 2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu alikemea vikali ucheleweshaji usiokuwa na sababu katika mchakato wa kupata idhini ya mikopo, ambapo miradi inaweza kuchukua hata mwaka mmoja kupitishwa kutokana na masharti na taratibu ngumu.

"Muhula wa pili wa awamu ya sita tutaanza kufanya miradi wenyewe halafu Mashirika yatatukuta njiani, tutakwenda nao. Hatutokaa kusubiri... mradi badala ya kupata approval miezi mitatu minne tunachukua mwaka mzima tunabembeleza mradi mmoja... Hatutosubiri hayo, tutaanza na fedha zetu za ndani."

 

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezungumza hayo leo Novemba 18, 2025 muda mfupi baada ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri wapya.

 

Ujumbe huu unaonesha uamuzi thabiti wa serikali kuondoa urasimu na kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa kasi ya hali ya juu kabla muda wa awamu hii haujaisha.