Jumatano , 10th Feb , 2016

Jeshi la Polisi Zanzibari limepiga marufuku vitendo vya kusambaza vipeperushi vyenye ujembe wa vitisho kwa wananchi vinginevyo sheria itachukua mkondo wake ili kudhibiti hali hiyo.

Kamishna wa Polisi Zanzibar Salim Msangi

Kamishna wa Polisi Zanzibar Salim Msangi amesema hayo jana wakati akiongea na waandishi wa habari visiwani humo na kusema kuwa kamwe jeshi la polisi haliwezi kukaa kimya juu ya vitendo hivyo vya vitisho.

Msangi amesema kuwa Zanzibar ni sehemu salama kama wananchi watafuata sheria na taratibu za nchi lakini wale wanaopanga kuvuruga amani iliyopo watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria bila kuonewa huruma.

Kamanda Msangi amesema baadhi ya vipeperushi hivyo vina ujumbe wa “One day Yes-iko siku itakua kweli” hivyo jeshi la linatoa tahadhari kwa mtu kwa mtu au kikundi au jumuiya inayohusika na kusambaza vipeperushi hivyo.

Akizungumzia Kikundi cha Mazombi ambacho kinadwaiwa kupiga raia wakiwa wamefunika sura zao amesema uchunguzi walioufanya umebaini kundi hilo halipo kwa sababu hakuna taarifa za watu waliofanyiwa vitendo hivyo katika jeshi hilo.