Jumamosi , 6th Jun , 2015

Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania NEC imesema imevuka malengo ya uandikashi wapiga kura kwa mfumo wa BVR katika mikoa ya Lindi, Ruvuma na Iringa ambayo wamemaliza uandikishaji mwezi uliopita.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania NEC imesema imevuka malengo ya uandikashi wapiga kura kwa mfumo wa BVR katika mikoa ya Lindi, Ruvuma na Iringa ambayo wamemaliza uandikishaji mwezi uliopita.

Akizungumza na EATV, Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA wa Tume hiyo, Dkt. Sisti Cariah amesema mkoani Lindi makairio yalikuwa kuandikisha watu 518, 230 lakini wameandikisha wapiga kura 569,261.

Ruvuma makadirio yalikuwa 783, 290 lakini walioandikishwa ni 826,779 wakati Iringa waliopangwa kuandishwa ni 525, 015 lakini walioandikishwa ni 526,006.

Kwa upande wa Mtwara Dkt Cariah amesema kuwa makadirio yalikuwa ni kuandikisha watu 703, 118 lakini walioandikishwa ni 682, 295.

Cariah amesema zoezi la uandikishaji linaendelea vizuri katika mikoa nane ya Katavi, Rukwa, Mbeya ,Dodoma ,Kagera ,Singida ,Tabora na Kigoma.

Amewataka wananchi kujiandaa kuandikishwa katika mikoa ya Mwanza, Geita, Shinyanga, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Shinyanga, Simiyu na Mara ambako zoezi hilo litaanza June 9, mwaka huu.

Jumla ya mikoa mitano imekwishakamilisha zoezi hilo, ambayo ni Mtwara, Lindi, Ruvuma, Iringa na Njombe.