Ijumaa , 24th Dec , 2021

Mkuu wa mkoa wa Geita Rosemary Senyamule, amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri kuwachukulia hatua maafisa ugavi na wahandisi wanaosimamia ujenzi wa vyumba vya madarasa yanayotokana na fedha za Uviko 19 baada ya kuzidisha makadirio ya vifaa na kuanza kutafuta wateja wa kuvinunua.

Mkuu wa mkoa wa Geita Rosemary Senyamule

Senyamule ametoa maagizo hayo wakati anakagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika halmashauri ya mji wa Geita, ambapo amekuta vifaa vinavyobaki baada ya ujenzi kukamilika ni mara mbili ya vifaa vilivyotumika.