Jumapili , 14th Aug , 2016

Chama cha Mapinduzi CCM kimesema kuwa katika chaguzi zote zilizowahi kufanyika hapa nchini uchaguzi wa mwaka jana ulikuwa ni mgumu katika michakato yake yote hadi kupatikana kwa Rais.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula

Kauli hiyo imetolewa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho upande wa Bara Philip Mangula wakati akizindua Daftari la Mashina ya chama hicho ambayo ndiyo chimbuko la wanachama wake kwa lengo la kuimarisha chama hicho na kuongeza wanachama.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika katika kijiji cha Utiga kata na halmashauli ya Wang'ing'ombe mkoani Njombe Mangula amesema kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa tofauti na miaka mingine ingawa kwa sasa ukirudiwa utakuwa rahisi.

Katika wilaya ya Wang'ing'ombe chama hicho kinadaiwa kuongoza kuwa na wanachama wengi na kupata madiwani wote wa CCM na kuwa sasa kinazindua kitabu hicho ili kuimarika zaidi.

Kitabu hicho kimezinduliwa pamoja na shina la chama hicho huku vitabu hivyo vikigawiwa kwa mabalozi 125 na viongozi wa kata 24 na wanachama lukuki wakijiunga na chama hicho na kukabidhiwa kadi za chama hicho na Mangula.

Sauti ya Philip Mangula, Makamu Mwenyekiti CCM, Bara
Sauti za Wanachama wa CCM, wilaya ya Wang'ing'ombe ambao ni: 1. JUMANNE KAPINGA - KATIBU CCM WANGING’OMBE 2. JOHARI MAIKO - MKAZI WANGING’OMBE 3. ROSE OSKA - MKAZI WANGING’OMBE 4. HAMIS NURDIN - MWASISI WANGING’OMBE