Jumatatu , 18th Aug , 2025

Isihaka Mchinjita, Makamu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Bara, akizungumza na SupaBreakfast ya EastAfricaRadio amesema kuwa wakati wa kampeni za ndani ya CHADEMA za kumtafuta Mwenyekiti, taswira ya chama iliharibika sana kutokana na makundi ya ndani kushambuliana vikali.

Ameeleza kuwa moja ya mambo yaliyoumiza zaidi ni namna kundi la Mbowe lilivyokuwa likimzungumzia Tundu Lissu, hadi kufikia hatua ya kumchukulia kama "mtu ambaye hafai hata kuwa mwenyekiti wa kijiji."