Jumatano , 3rd Jun , 2015

Chama cha Mapinduzi CCM kimetangaza ratiba ya uchukuaji fomu za kugombea nafasi hiyo kesho/leo kwa makada waliotangaza nia ambapo makada watano watapata fursa ya kuchukua fomu hizo na kwenda kutafuta wadhamini.

Kiny'ang'anyiro cha kuwania urais ndani ya chama cha mapinduzi CCM kinazidi kupamba moto baada ya chama hicho kutangaza ratiba ya uchukuaji fomu za kugombea nafasi hiyo kesho/leo kwa makada waliotangaza nia ambapo makada watano watapata fursa ya kuchukua fomu hizo na kwenda kutafuta wadhamini.

Akitangaza ratiba hiyo katibu wa halmashauri kuu ya taifa NEC idara ya oganaizesheni Mohamed Seif Khatib amewataja watangazania watakaoanza kuchukua fomu ni Profesa Mark Mwandosya akifuatiwa na Steven Wassira na kisha atachukua Edward Lowasa na baadae Amina Salum Ally na kisha atamalizia Makongoro Nyerere.

Seif Khatib akabainisha kuwa kila mgombea atatakiwa kutumia muda usiozidi saa moja na nusu kuchukua fomu na kuzungumza na vyombo vya habari huku wakiruhusiwa kuingia wasindikizaji wasiozidi kumi katika zoezi la uchukuaji litakaloanza saa nne kamili asubuhi na kumalizika saa kumi na kusu alasiri

Baada ya kuchukua fomu hizo wagombea watatakiwa kuzunguka katika mikoa 15 mitatu kati yake ya tanzania zanzibar ambapo wadhamini watakaojitokeza watatakiwa kuandika majina yao kamili na namba za kadi zao za uwanachama wa CCM kwenye fomu hiyo huku pia ikitakiwa kusainiwa na katibu wa ccm wa wilaya husika pamoja na kupigwa muhuri .

Ratiba hiyo itaendelea kutolewa kadiri watangaza nia watakavyopeleka maombi yao kuanzia tarehe 3 Juni mpaka tarehe 2 Julai ambayo ndio itakuwa tarehe ya mwisho ya kurudisha.