Jumanne , 7th Dec , 2021

Kampeni ya Namthamini 2021 imefanikiwa kugawa taulo za kike kwa wanafunzi wenye uhitaji katika Shule ya Msingi ya Uhuru Mchanganyiko iliyopo Ilala Jijini Dar es Salaam. 

Wanafunzi wa shule ya Uhuru Mchanganyiko wakifurahi na mtangazaji Vaniladama

Msaada huo umewafikia jumla ya wanafunzi 54 ambao sasa wataweza kusoma bila kikwazo cha kukosa taulo za kike kwa mwaka mzima.

Kampeni ya Namthamini ya East Africa Tv na East Africa Radio kwa kushirikiana na Flaviana Matata Foundation inalenga zaidi katika kusimamia ustawi wa mtoto wa kike hasa katika masomo yake kwa kumsaidia katika kipindi cha hedhi asiweze kukosa masomo.