Alhamisi , 7th Aug , 2014

Wakazi wa vijijini wapatao milioni 2 kutoka maeneo mbalimbali nchini Tanzania wanatarajiwa kuanza kunufaika na huduma ya maji safi na salama ifikapo Desemba mwakani.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Jumanne Maghembe.

Huduma hiyo ya maji itapatikana kufuatia msaada wa Pauni za Uingereza milioni 150 zilizotolewa na serikali ya Uingereza kwa serikali ya Tanzania.

Akizungumza mara baada ya msaada huo Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe amesema msaada huo umekuja kwa wakati mwafaka, ambapo wizara yake imeelekeza nguvu vijijini, hivyo kupitia msaada huo kutaharakisha utekelezaji wa mpango wa matokeo makubw sasa BRN.

Profesa Maghembe amebainisha utekelezaji wa miradi ya maji vijijini na usafi wa mazingira na mpango wa matokeo makubwa sasa kuwa umesaidia sana kuondoa magonjwa sumbufu yaliyokuwa wakiwasumbua wananchi waishio vijijini.