Jumapili , 21st Mar , 2021

Makamu wa Rais wa Marekani Bi. Kamala Harris amemtumia salamu za pongezi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan baada ya kuapishwa kwake kuwa rais kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais Dkt. John Magufuli Machi 17, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa ‘twitter’ Kamala amemhakikishia Rais Samia ushirikiano ili kuendelea kuimarisha mahusiano yaliyopo baina ya nchi hizo, sambamba na kumpongeza kwa kuwa Rais wa kwanza Mwanamke Tanzania.

Nina mtakia kila la kheri Samila Suluhu Hassan kufuatia kuapishwa kwake kuwa Rais mpya wa Tanzania na mwanamke wa kwanza kuongoza ofisi hiyo. Marekani ipo tayari kufanyakazi na wewe ili kuimarisha uhusiano baina ya nchi zetu,” ameandika Kamala.