Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Amesema Watanzania wa leo wanataka kusikia maendeleo na sio kuburuzwa kama zamani, na kudai kuwa kwa sasa kutengeneza matukio ni kuharibu maisha ya watu.
''Unatengeneza tukio hapa la ajabu halafu useme fulani ndiyo kafanya, kumbe siyo aliyefanya haina maana, unapoteza miundombinu,unaharibu maisha ya watu, unaleta tafrani kwenye jamii'', amesema Majaliwa.
"Watanzania sasa hivi sio watu wa kuambiwa tu na kuburuzwa nenda mkaandamane yeye mwenyewe amekaa tu, tunamuona kwenye televisheni haendi kuandamana ,twende na utangulie, kiongozi ndiyo anatangulia hawa sio Watanzania wa juzi, leo Watanzania wanatakiwa kusikia maendeleo'', ameongeza.
Aidha amewataka Watanzania kujitokeza kwenda kutumia haki yao ya Kidemokrasia kwa kumchagua kiongozi wanaemtaka atakaye waletea maendeleo.






