
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo
Kauli hiyo ameitoa hii leo Desemba 8, 2021, Dar es Salaam, wakati akizungumzia mafanikio yaliyopo baada ya miaka 60 ya Uhuru, wapi walikotoka na wapi ilipo serikali inayoongozwa na chama hicho, huku akiahidi kwamba chama hicho kitaendelea kujenga Tanzania imara katika nyanja mbalimbali za amendeleo.
"Nchi yetu wakati inapata Uhuru, upatikanaji wa maji katika miji yetu ulikuwa kwa asilimia 25 tu kuna miji ilikuwa inapata maji kwa asilimia 8, 6 ama 10, lakini leo miaka 60 baada ya Uhuru upatikanaji wa maji ni asilimia 86, tuko kwenye kiwango kizuri," amesema Chongolo.