Jumapili , 31st Mar , 2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi, utenguzi na uhamisho wa viongozi kama ifuatavyo:

Amemteua Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb.) kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu). Kabla ya uteuzi huu Mhe. Ndejembi alikuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI). Mhe. Ndejembi anachukua nafasi ya Mhe. Prof. Joyce Lazaro Ndalichako ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Amemteua Bw. Paul Christian Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Kabla ya uteuzi huu Bw. Makonda alikuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM). Anachukua nafasi ya Mhe. John Vianney Mongella ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Amemteua Kanali Evans Alfred Mtambi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara. Kabla ya uteuzi huu Kanali Mtambi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga.

Amemhamisha Mhe. Said Mohamed Mtanda kutoka Mkoa wa Mara kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. Mhe. Mtanda anachukua nafasi ya Mhe. Amos Gabriel Makalla ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Amemteua Mhe. Zainab Athuman Katimba (Mb.) kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa ana Serikali za Mitaa (TAMISEMI). Mhe. Zainab anachukua nafasi ya Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb.) ambaye ameteuliwa kuwa Waziri.

Amemteua Mhe. Daniel Baran Sillo (Mb.) kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Mhe. Sillo anachukua nafasi ya Mhe. Jumanne Abdallah Sagini (Mb.) ambaye amehamishwa kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria.

Amemhamisha Mhe. Mhandisi Maryprisca Winfred Mahundi (Mb.) kutoka Wizara ya Maji kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Amemhamisha Mhe. Kundo Andrea Mathew (Mb.) kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Maji.

Amemteua Bw. Fakii Raphael Lulandala kuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro. Kabla ya uteuzi huu Bw. Lulandala alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM).

Amemteua Bw. Gilbert Kalima kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga. Kabla ya uteuzi huu Bw. Kalima alikuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi.

Amemhamisha Mhandisi Cyprian John Luhemeja kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu) kwenda kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Amemhamisha Bi. Mary Ngelela Maganga kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kwenda kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).

Amemteua Dkt. Edwin Paul Mhede kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi. Dkt. Mhede aliwahi kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART).

Dkt. Mhede anachukua nafasi ya Bi. Agnes Kisaka Meena ambaye amehamishwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji.

Amemteua Dkt. Suleiman Hassan Serera kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. Kabla ya uteuzi huu Dkt. Serera alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro.

Dkt. Serera anachukua nafasi ya Bw. Nicholaus Mkapa ambaye amehamishwa kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia wa Habari.

Amemteua Bw. Selestine Gervas Kakele kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huu Bw. Kakele alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Amemteua Balozi Dkt. Asha Rose Migiro kuwa Mjumbe wa Tume ya Mipango.

Uapisho wa Waziri, Wakuu wa Mikoa, Naibu Mawaziri na Naibu Makatibu Wakuu utafanyika tarehe 04 Aprili, 2024 saa 05:00 asubuhi Ikulu, Dar es Salaam.