Mama akiwa amembeba mtoto wake aliezaliwa kabla ya wakati kwa mtindo wa Kangaroo
Dawa hizo zinatajwa kuwa zitapunguza vifo vya watoto hao ambao wengi wao hupoteza maisha wakiwa njiani kuwahishwa katika hospitali ya taifa Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa huduma hiyo
Wakizungumza katika hospitali ya wilaya ya Kisarawe baadhi ya akina mama waliojifungua hivi karibuni wamesema ujio wa dawa hiyo pamoja na uboreshwaji wa huduma ya mama na mtoto kumesaidia kupunguza adha waliyokua wakiipata na sasa wanaishukuru serikali ya mama Samia Suluh Hassan kwa kazi kubwa ya kuimarisha sekta ya afya nchini
Kwa upande wake mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Kisarawe Dk. Zaitun Hamza amesema hospitali imekua ikipokea fedha kila mara kwaajili ya kununulia dawa huku madaktari bingwa wa magonjwa ya akina mama na watoto wakielezea ujio wa dawa ya Surfactant itakavyosaidia kupunguza vifo vya watoto wanaozaliwa chini ya wiki 32.
