Ijumaa , 12th Aug , 2022

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya vijana duniani imeelezwa kuwa zaidi ya vijana laki nane wanaoingia mtaani kila mwaka wamekuwa wakikosa ajira huku changanoto ikiwa ni vijana kukosa elimu ya kujitegemea pamoja na changanoto nyingine katika masuala ya uongozi pamoja na ukatili

Kaimu Mkurugenzi  wa Chemba ya Kilimo na Biashara (TCCIA) Nerbat Mapwele

Akizungumza  leo katika jukwaa la vijana wa Afrika Mashariki  Kaimu Mkurugenzi  wa Chemba ya Kilimo na Biashara (TCCIA) Nerbat Mapwele amesema bado vijana wa Afrika Mashariki wana kabiliwa na changanoto nyingi ikiwemo katika ajira, ukatili wa kingonon kupitia  mitandao ambao umekuwa ukiathiri vikubwa makundi ya vijana na kushindwa kufikia malengo yao.

Kwa upande wake Balozi wa vijana Afrika mashariki Jescca  Mshama amesema katika jukwaa hilo vijana wamekutana na kujadili masuala mbalimbali ikiwemo changamoto katika uongozi, ajira na masuaka ya ukatili wa kijinsia