Jumamosi , 13th Nov , 2021

Kamanda wa Polisi wilaya ya Kisarawe Eva Steshen, amesema vijana wanashindwa kuoa mapema kwa sababu huduma ambayo walipaswa kupatiwa na wake zao baada ya kuoa wamekuwa wakiipata kwa bei nafuu kutoka kwa wadada poa wanaofanya biasahra ya ngono wilayani humo.

Kamanda wa Polisi wilaya ya Kisarawe, Eva Steshen

Kauli hiyo imetolewa wakati wa ziara iliyofanywa na kamati ya UKIMWI iliyobaini kuwepo kwa madanguro na madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo wakasema hawatowafukuza bali wamewawekea mpango wa kuwapatia elimu ya ujasiriamali wasichana hao pamoja na kuwapatia mikopo kama mitaji itakayowawezesha kuachana na vitendo vya ukahaba.