Alhamisi , 7th Dec , 2017

Mawakala na viongozi wa CHADEMA waliokamatwa wakati wa uchaguzi mdogo wa marudio Novemba 26 wameshindwa kufikishwa mahakamani leo kwa kukosa polisi wa kuwasindikiza.

Kupitia Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche amethibitishwa kutopelwekwa mahakamani kwa watu hao na kusema kwamba ni muendelezo wa kucheza na haki za binadamu.

Heche amesema kwamba "Mawakala na viongozi wetu waliokamatwa tarehe 26 kunyimwa dhamana hapa Maswa wameshindwa kuletwa mahakamani leo tena ambayo ndio ilikua siku ya kesi. 

"Kwa kisingizio cha kukosa polisi wa kuwaleta huu ni muendelezo wa utaratibu wa kucheza na haki za watu ,mapambano yanaendelea" Heche