
Mamlaka zinasema kwamba vipodozi hivyo vina vitu vinavyoweza kusababisha saratani, pamoja na kuwa na madhara kwa afya ya uzazi na uwezekano wa kusababisha utasa.
Sheila Mercis, ambaye ni mkaguzi katika mamlaka ya udhibiti wa dawa nchini humo amesema kwamba Umoja wa Ulaya ulikuwa umeonya dhidi ya bidhaa hizo mapema mwezi Septemba.
Amesema kwamba ili kudhibiti uingizwaji wake, mamlaka inahakikisha kwamba katika soko, angalau, hakutakuwa tena na bidhaa za kuuza.
Watengenezaji tayari wamewasilisha fomula mpya za vipodozi vinavyohusika kwenye mamlaka hizo kwa idhini ili ziweze kuingizwa tena "bila ya kuwa na vitu vyenye madhara".
Wazalishaji wote barani Ulaya tayari wameondoa kemikali zenye madhara.