Kufuatia mgogoro unaondelea ndani ya chama cha ADC, Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini imethibitisha kupokea taarifa za mgogoro huo na tayari ofisi hiyo imeanza kulifanyia kazi suala hilo.
Akizungumza na East Africa Television Msajili msaidizi wa vyama vya siasa nchini Dkt.Sisty Nyahoza amesema ofice ya msajili imejirithisha kuwa ni kweli kwamba mwenyekiti wa Taifa wa ADC Bwana Miraji alilumbana na mlezi wa chama hadi kufikia hatua ya kutoa taarifa kwenye vyombo vya habari.
Amesema ni kweli kwamba hali hii inawezekana kuichafua taswira ya chama kwa jamii lakini ofisi haijaona sehemu mahususi katika katiba ya ADC inayoonyesha kuwa kufanya hivyo ni kukiuka Katiba ya chama na bodi ya wadhamini hawajawasilisha maelezo yoyote kuthibitisha kuwa kwa kufanya hivyo mwenyekiti alivunja katiba ya chama.......Footage.....
Dr.Nyahoza ameviasa vyama vya siasa kufuata katiba na sheria ya vyama vyao wanazoziweka ili kuhakikisha wanaachana na migogoro inayojitokeza mara kwa mara.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama hicho ambaye analalamikiwa na wanachama Bwana Saidi Miraji amesema yeye anaongozwa na katiba iliyopitishwa na chama chake kwakua kila jambo ndani ya chama hicho katiba na sheria ndio muongozo halali wakuufuatwa na sio maneno yawanachama pembeni na makubaliano yaliyopitishwa kwenye katiba.
