Jumanne , 25th Oct , 2022

Jeshi nchini Sudan limefyatua gesi ya kutoa machozi katika jaribio la kuwazuia maelfu ya waandamanaji kuandamana kuelekea ikulu ya rais.

Maandamano hayo yanafanyika kote nchini humo kuadhimisha kumbukumbu ya kwanza ya mapinduzi yaliyositisha kipindi cha mpito cha kidemokrasia.

Tangu mkuu wa jeshi, Abdel Fattah al-Burhan, alipotwaa madaraka kumekuwa na maandamano ya karibu kila wiki ya kupinga mapinduzi.

Vikosi vya usalama vimeshutumiwa kwa kuwaua zaidi ya waandamanaji 100 katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Kutwaa madaraka kwa jeshi kulisababisha wafadhili wa kigeni kukata msaada na uchumi wa Sudan umekuwa katika machafuko.