Jumanne , 31st Mei , 2016

Bunge limetoa maazimo ya kuwaadhibi wabunge sita wa Kambi ya Upinzani kutokana na vurugu na utovu wa nidhamu na kutoheshimu kiti wakati wa mjadala wa kujadili bunge kwenda live.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto Zuberi Kabwe akiteta Jambo la Mbunge Tundu Lissu

Akisoma azimio hilo Mwenyekiti wa Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Mhe. George Mkuchika, amewataja wabunge hao kuwa ni Mhe. Esther Bulaya, na Mhe. Tundu Lissu ambao wametakiwa waisihudhurie vikao vilivyobaki vya bajeti na mkutano wa nne.

Wengine ni Zitto Kabwe, Godbless Lema, Halima Mdee, na Pauline Gekul wamefungia kushiriki vikao vilivyobaki vya bajeti ambapo John Heche amefungiwa kushiriki vikao kumi mfululio.

Katika Hatua nyingine Kambi Rasmi ya Upinzani imesema imepangilia kumjadili na kumkataa Naibu Spika wa Bunge hilo Mhe. Tulia Ackson Kwa kushindwa kuhimili kuliendesha bunge hilo.

Akiongea na waandishi wa Habari jana Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Mhe. Freeman Mbowe, wamesema kwa kuonyesha kumkataa kiongozi huyo watakuwa wanatoka kila Naibu Spika huyo atakapokalia kiti.