Wabunge wanne CHADEMA waibuka CCM

Alhamisi , 15th Nov , 2018

Wabunge wanne waliokuwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA na baadaye kuhamia CCM na kushinda nafasi zao ubunge wameapishwa leo bungeni na Spika wa Bunge Job Ndugai na kuanza kuzitumikia nafasi hizo tena kupitia chama kingine.

Chama Cha Demokrasia na Maemdeleo (CHADEMA)

Miongoni mwa wabunge hao walioapishwa ni Mbunge wa Babati Mjini Pauline Gekul, Mbunge wa Simanjiro James Ole Milya, Mbunge wa Ukerewe Joseph Mkundi pamoja na Mbunge wa Serengeti Marwa Ryoba.

Wabunge hao walikuwa ni wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, wakihudumu kwenye chama hicho kwa kipindi cha miaka 2 na nusu lakini baadaye walihama kutokana sababu mbalimbali ikiwemo kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli.

Akijibu swali la kwanza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amewapongeza wabunge hao na kuwataka kutekeleza majukumu yao ya kihalali ya kuishauri serikali.

Nawapongeza wabunge wapya walioapishwa leo nawakaribisha hapa, mtekeleze majukumu yenu kama wabunge na sisi kama serikali tuko tayari kuwasikiliza” amesema Waziri Mkuu.