Jumatano , 3rd Jun , 2015

Waziri mkuu wa Tanzania Mh Mizengo Pinda leo amewaongoza wabunge wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuaga mwili wa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Ukonga jijini Dare s salaam Marehem Eugen Mwaiposa.

Waziri mkuu wa Tanzania Mh Mizengo Pinda leo amewaongoza wabunge wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuaga mwili wa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Ukonga jijini Dare s salaam Marehem Eugen Mwaiposa, aliyefariki jana nyumbani kwake mjini mjini Dodoma.

Shughuli ya kuaga mwili wa mbunge huyo imefanyika leo mchana nyumbani kwa mbunge huyo maeneo ya Chadulu mjini Dodoma, na kuhudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa madhehebu ya dini na serikali akiwemo mkuu wa mkoa wa Dodoma, Kepteni mstaafu Chiku Galawa.

Katika salamu zake kwa niaba ya Bunge, Naibu Spika wa bunge Mh. Job Ndugai ameuelezea msiba kuwa ni pigo kwa bunge na taifa kiujumla, kwa kuwa mambo mengi mazuri aliyokuwa nayo marehemu bado yalikuwa yanahitajika.

Kwa upande wao baadhi ya wabunge waliohudhuria shughuli hiyo kwa uwakilishi wa makundi yao wamesema watamkumbuka marehemu kwa mengi ikiwa ni pamoja na uwezo wake wa kusimamia hoja mbalimbali za maendeleo katika jimbo lake.

Baada ya shughuli ya kuaga, mwili wa marehemu Mwaiposa umesafirishwa kutoka Dodoma kwa njia ya Ndege na umewasili alasiri nyumbani kipunguni Dar es salaam tayari kwa maziko ambayo yatafanyika siku ya Jumamosi hapo hapo Kipunguni Dar es salaam.

Tags: