Alhamisi , 3rd Sep , 2020

Jeshi la zimamoto na Uokoaji limetoa onyo kwa wafanyabiashara ambao huuza vifaa vya kuzimia Moto pasipo kuwa na kibali ama usajili maalum kwa kuwa vingine huuzwa vikiwa muda wake wa matumizi umeisha hivyo kuleta Adha kwa wananchi.

Rai hiyo imetolewa na Kamanda wa Mkoa wa Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa kizima moto Ilala mrakibu Msaidizi Elisa Mugisha Katika onesho maalum la jinsi gari yenye ujazo wa lita Elfu saba inavyomaliza maji kwa dakika chache hali ambayo mara nyingi huzua maswali mengi kwa wananchi pindi yatokeapo majanga.

" Leo tunataka jamii ya watanzania ijue kwamba gari yetu haiwezi kutoka kituoni bila kuwa na maji hii ni swali tuu ambalo wananchi wamekuwa wakiuliza na kusambaza kitu ambacho hakina ukweli Pana sababu nyingi za gari kumaliza maji kwa haraka ikiwemo aina ya moto wenyewe ambayo italazimisha kutumia njia nyingi,Kasi ya maji kubwa Ili kuzima moto kuwa haraka,hivyo wananchi wanatakiwa kuyajua haya"alisema ELISA MUGISHA-Mrakibu Msaidizi Jeshi la zimamoto na uokoaji Ilala.

Kamanda Elisa emesema kwa wafanya biashara ambao watabainika hawana usajili hatua kali za Kisheria zitachukiliwa dhidi yao kwa kuwa vifaa vya maokozi ni sio Kama bidhaa nyingine akiiasa jamii pia kuwa na tabia ya kusoma mwisho wa matumizi ya kifaa anachotaka kununua.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wamesema Hali hiyo inatokana na taharuki ambayo inakuwa imetanda mtaani kw a wakati wa majanga kiasi ambacho wengi hawajui masuala hayo ya kitaalam kuwa nini kinamaliza maji Ili hali gani inaonekana ni kubwa.