
Wafanyabiashara wa Kuku katika soko la Buguruni Jijini Dar es salaam wanaiomba serikali kuweka mazingira mazuri ya kuwapatia chanjo kuku na kutoa ushauri kwa wafugaji ili waweze kukuza kuku vizuri na kuweza kujipatia kipato kutokana na biashara hiyo.
Wakiongea na East Africa Radio hii leo Wafanyabiashara wametoa kauli hiyo kufuatia upungufu mkubwa wa kuku katika soko hasa katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za pasaka hali iliyosababishwa na kuku wengi kufa katika maeneo ambayo wanazalishwa kutokana na magonjwa kama mdondo na mafua
Aidha wamebainisha kuwa hali hiyo imepelekea bei ya kuku kupanda na kuwafanya walaji kushindwa kumudu gharama za kuku na kuwapelekea ugumu wa maisha kwa wafanyabiashara wenyewe na familia wanazozihudumia.