Jumatatu , 6th Mar , 2023

Waganga wa jadi na tiba asili Mwanza wamemuomba kamanda wa polisi wa mkoa huo Wilbroad Mutafungwa kuwachunguza askari polisi wanaofanya msako wa waganga wasio waaminifu wanaopiga ramli chonganishi na kusema wapo baadhi ya maaskari ambao hushirikiana na waganga hao kujiingizia kipato

Waganga hao wanasema kuwa baadhi ya polisi huwakamata  waganga wenye sifa na kuwatoza fedha

Kauli hiyo wameitoa kwenye kikao maalum cha amani na usalama kilichowakutanisha waganga hao wa jadi pamoja na jeshi la polisi mkoani Mwanza lengo likiwa ni kuweka mikakati ya kupunguza matukio ya mauaji katika mkoa huo
"Kwa sababu ilifikia hatua hata wizara ya afya jeshi la polisi wanapoingia oparesheni wanakamata hata kama una kibali wanakificha unakamatwa"

"Mheshimiwa naomba ujue kwenye jeshi lako la polisi kuna watu siyo waaminifu wanshilikiana na wahuni matapeli kupointi watu muhimu ili tuje tukamatwe ili wapate pesa juzi imetokea Igoma ilikuwa mzee wangu afungwe mzee wangu Hmais aanauza madawa nauzia waganga anasaidia watu kwa uhuru amechomewa maneno kwenye kituo cha polisi kishiri kwamba anauza dawa za uwongo anauza majivu"

"Lakini hatujawahi kuona mambo ya mauaji hamna mandago ya kutoa damu ya mtu tunashukuru seriklai imetueleza na sisi tutaenda kuweka kikao kwetu"

Akiwa kwenye kikao hicho kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa akawataka waganga hao kuendelea kutoa taarifa pindi wanapowabaini wahalifu na maaskari wasio waaminifu ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao

"Na ikitokea umetoa taarifa mtu amechukuliwa halafu ukao kuna sintifahamu inaendelea huko pengine kuna askari ambae siyo mwaminifu pia piga simu kwa mkuu wa polisi wa wilaya, mkuu wa upelelezi wa mkoa au mkuu wa polisi wa mkoa ambao tutatoa namba zao za simu ili na yule polisi ambae ameingia kwenye janja janja nay eye achukuliwe hatua lakini pia tukipata taarifa yam ganga kumuhifadhi mhalifu tutakuja kumkamata mhalifu lakini na wewe pia hatutakuacha"