Wagonjwa hao watapatiwa matibabu kupitia mradi wa ujenzi wa Kliniki hizo unaotekelezwa na shirika la Kikorea la Heart to Heart Foundation.
Akizungumza leo mkoani Mtwara katika hafla ya uzinduzi wa jengo la Kliniki hiyo, mkurugenzi wa shirika hilo, Grece Lee, amesema jengo hilo lililogharimu zaidi ya dola za Kimarekani 110,000 tayari limekamilika likiwa na vifaa vya kisasa kwa ajili ya kutoa huduma za upasuaji wa macho (Mtoto wa Jicho).
Mratibu wa huduma za macho katika mkoa wa Mtwara, Dkt. Upendo Abeid, amesema jamii ya mkoani hapa bado ina uelewa mdogo juu ya ugonjwa huo ambao unaweza kupelekea kuwa kipofu iwapo utachelewa kupata tiba.
Athuman Bakari, ni mmoja wa watu waliowahi kuugua ugonjwa huo kwa kipindi kirefu na kumfanya ashindwe kuona vizuri, lakini kwa sasa amepona tatizo hilo baada ya kupata matibabu kutoka kwa wataalamu kupitia hospitali ya Ligula.