Ijumaa , 7th Oct , 2022

Wajumbe wa kamati ya ushauri ya mkoa wa Mtwara (RCC) wamesema hawana imani na mkandarasi  anayetekeleza mradi wa REA  awamu ya kwanza mzunguko wa tatu, kutokana na mkandarasi huyo kushindwa kutekeleza mradi huo kwa wakati

Wakati serikali ikipambana kuahakikishwa kwamba wananchi   wanaoishi wa vijijini wanapata umeme, imeelezwa kuwa mkandarasi  anayetekeleza  mradi wa umeme katika wilaya ya Tandahimba na Newala, central internation l.t.d ameshindwa  kukamilisha mradi kwa wakati ambapo wajumbe wa kikao hicho wamedai kutokuwa na Imani mkandarasi huyo.

Uzinduzi wa REA awamu ya kwanza mzunguko wa tatu,  Mkoani Mtwara, mwaka jana katika Kijiji cha  Namtumbuka halmashauri ya mjini Nanyumba na kuhudhuliwa na aliyekuwa  Waziri wa Nishati  Medard  Kalemani