Jumatano , 1st Dec , 2021

Watu wawili wakazi wa Dar es Salaam, wamekamatwa na Jeshi la Polisi Kikosi cha Viwanja vya Ndege, baada ya kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroin katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, baada ya kuwasili na ndege ya Fly Dubai wakitokea nchini India.

Kamanda wa Polisi Kikosi cha Viwanja vya Ndege Tanzania ACP Jeremia Shila

Taarifa hiyo imetolewa leo Desemba 1, 2021, na Kamanda wa Polisi Kikosi cha Viwanja vya Ndege Tanzania ACP Jeremia Shila, na kusema kwamba dawa hizo walikuwa wamezificha chini ya mabegi yao ya nguo, ambapo mmoja ni mkazi wa Mbagala na mwingijne ni mkazi wa Tabata, na wote kwa pamoja wamekamatwa na dawa zenye uzito wa kilogramu 7.116 aina ya heroin.

Watu hao wamekamatwa kwa ushirikiana na vyombo vingine vya usalama.